WAKATI WA MAPUMZIKO KAZI IENDELEE

    WAKATI wa mapumziko wachezaji wengi wamekuwa wakiendelea na maisha ya kawaida nje yay ale waliyokuwa wakiishi walipokuwa kambini ama wakati wa maandalizi ya mechi za kitaifa na kimataifa.

    Singida Fountain Gate hawa wapo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku Yanga na Simba wakiwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Kazi yao inapaswa kuwa kubwa kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.

    Sio kila timu zimevunja kambi wapo ambao wamerejea kambini wakiendelea na maandalizi kwa mechi zinazofuata.

    Ligi imesimama kwa muda kutokana na majukumu ya timu ya taifa kuwania kufuzu AFCON. Haina maana kwamba muda wa mapumziko na maisha ya mpira nayo yapelekwa likizo.

    Benchi la ufundi huwa linatoa program maalumu kwa wachezaji ili wazifuate wakati wa mapumziko hivyo ni muhimu nidhamu kuzingatiwa kwenye kutimiza majukumu hayo.

    Ikiwa kila mchezaji atafuata kile anachoambiwa itakuwa kazi nyepesi watakaporejea mazoezini kutambua wapi wataanzia kwa ajili ya kuendelea kuyakimbiza malengo yao.

    Kila kitu kinahitaji muda na umakini kwenye kutimiza maelekezo ya benchi la ufundi kwa wale wachezaji ambao watapuuzia haitakuwa afya kwao wala timu kiujumla.

    Inawezekana kurejea kambini ukiwa imara na kuruhusu kazi ya kusaka ushindi kuendelea kama wachezaji watafuata kile walichoambiwa na benchi la ufundi.

    Muda ni sasa na kila kitu kinawezekana kwa kuzingatia maelekezo na kuyafuata bila kukata tamaa kwa kuwa ligi haitasimama muda wote itaendelea.

     

    Previous articleKILA LA KHERI WACHEZAJI WA TAIFA STARS
    Next articleYANGA KAZI BADO INAENDELEA