Home International KILA LA KHERI WACHEZAJI WA TAIFA STARS

KILA LA KHERI WACHEZAJI WA TAIFA STARS

WACHEZAJI ambao wamepewa kazi ya kupeperusha bendera ya Tanzania katitka timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuna kazi kubwa kubwa ambayo mnapaswa kuifanya kwenye mchezo wa leo.

Ukweli ni kwamba Watanzania wanamatumaini makubwa na kazi yenu ambayo haitakuwa nyepesi ndani ya dakika 90 kwa kuwa mpira ni mchezo wa makosa.

Kikubwa ambacho kinatakiwa kwenye mchezo wa leo wachezaji kujitoa kwa hali na mali kusaka ushindi kwa kuwa hiyo itakuwa furaha ya Tanzania kiujumla.

Kambi ile ya mapema ambayo iliwekwa  nchini Tunisia ikiwa ni maandalizi ya kueleka mchezo wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Algeria majibu yake yanasubiriwa na mashabiki pamoja na benchi la ufundi.

Ukweli ni kwamba wachezaji wanatambua kwamba mechi za kimataifa ni ngumu kutokana na kila timu kutafuta ushindi. Hiyo ni mbinu ya ushindi kwa kila mchezaji kujitoa kwa asilimia kubwa kutafuta ushindi.

Inawezekana kupata ushindi ugenini na kurejea nyumbani mkiwa na zawadi kubwa ambayo itakuwa ni furaha kwa kila mmoja.

Makosa ambayo yalitokea kwenye mechi zilizopita yafayiwe kazi kwenye upande wa kutengeneza nafasi na kuzitumia kwani ni ngumu kuzitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo mmoja.

Mashabiki waliopo Tanzania silaha kubwa iwe kwenye dua njema kwa wachezaji wafanye kazi kwa umakini na kupata matokeo mazuri.

Previous articleHUYO KRAMO ANA BALAA KWELI HUKO
Next articleWAKATI WA MAPUMZIKO KAZI IENDELEE