SIMBA: MATOKEO MABAYA, HASIRA KUHAMIA HUKU

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa matokeo waliyopata dhidi ya CS Constantine ni mabaya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuwa walifanya makosa ndani ya dakika tano ambayo yaliwagharimu.

Kwenye mchezo uliochezwa Desemba 8 2024 Simba walitangulia kufunga dakika ya 24 kupitia kwa Zimbwe na walifungwa mabao mawili kipindi cha pili dakika ya 47 kwa beki Hamza kujifunga na dakika ya 51 kupitia kwa nahodha wa CS Constantine, Jian.

Ahmed amesema: “Matokeo tuliyopata dhidi ya CS Constantine ni mabaya na kilichotokea hatuwezi kubadili sasa ni hesabu kuelekea mchezo wetu wa tarehe 15 ambapo tutakuwa nyumbani kwenye mchezo wa hatua ya makundi.

“Kikubwa kuelekea kwenye mchezo wetu mashabiki tuungane kwenye kampeni za kusaka ushindi kwani matokeo yaliyopita tukiwa nyumbani tulipata pointi tatu na sasa ni kuelekea mchezo wetu wa pili tukiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa.”

Katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya CS Constantine baada ua dakika 90 ubao ulisoma CS Constantine 2-1 Simba na bao la Simba likifungwa na Mohamed Hussen dakika ya 24 ambaye ni nahodha.

Mchezo huo itakuwa ni dhidi ya CS Sfaxine iliyotoka kupoteza kwa kufungwa mbaoa 3-1 dhidi ya Bravos wote wakiwa kundi A ambalo vinara ni CS Constantine yenye pointi sita.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.