Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Uhispania, Rodrigo Hernández Cascante almaarufu Rodri ameshinda tuzo ya Ballon d’Or 2024 aliwabwaga Vinicius Jr na Jude Bellingham.
Rodri anakuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England kushinda Ballon d’or tangu Cristiano Ronaldo alipofanya hivyo mnamo 2008.
Rodri ni kiungo wa kwanza kutwaa tuzo hiyo tangu Luka Modric 2018.
Rodri ndio mchezaji wa kwanza wa Manchester City kushinda tuzo hiyo kihistoria.