USIKU wa tuzo kubwa duniani ambazo zilikuwa zinasubiriwa kwa shauku bila uwepo wa majina ya mastaa wakubwa CR 7 na Messi umegota mwisho na majibu yamepatikana kwa mshindi kuwa wazi tofauti na wengi walivyokuwa wakitarajia awali.
Kiungo wa Man City ambaye anacheza katika kikosi cha Manchester City, yeye ni raia wa Hispania anaitwa Rodri ametangazwa kuwa mshindi wa Ballond’Or 2024.
Wakati yeye akiwa namba moja nafasi ya pili imekwenda kwa Vinicius Jr ambaye huyu alikuwa akipewachapuo kuwa huenda akatwaa tuzo hiyo na mwisho mambo yamekuwa tofauti kwake tuzo ikienda kwa mwamba Rodri huku namba tatu akiwa ni Jude Bellingham, wote kutoka Real Madrid.
Timu bora upande wa Klabu ni Real Madrid, kocha bora ni Carlo Anceloti wa Real Madrid na mlinda mlango bora wa dunia anaitwa Emiliano Martinez wa Aston Villa raia wa Argentina.
Aliyechukua Ballon d’Or upande wa soka la wanawake ni Aitana Bonmati wa Barcelona raia wa Hispania na sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilifanyika usiku huu, Paris nchini Ufaransa.