YANGA WAIKANDA MKONO ASAS DJIBOUT LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  IKIWA Uwanja wa Azam Complex imeshuhudia ubao ukisoma Yanga 5-1 ASAS FC mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

  Ushindi huo unaipa nafasi Yanga kusonga mbele hatua inayofuata ambapo unatarajiwa kumenyana na Al Merreikh ya Sudan.

  Mabao ya Yanga yamefungwa na Max Nzengeli aliyetupia mara mbili dakika ya 7, 90 huku Konkoni akitupia dakika ya 45 Zouzoua akitupia dakika ya 55 na Clement Mzize ni dakika ya 69.

  Bao la ASAS FC limefungwa na Tito Mayor kwa penalti dakika ya 85. Inasonga mbele Kwa ushindi wa jumka ya mabao 7-1.

  Katika mchezo wa leo Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alianza na beki Kibwana Shomari na Nickson Kibabage kwa upande wa kumwaga majalo.

  Previous articleYANGA 2-0 ASAS DJIBOUT
  Next articleBETO YA VIUNGO SIMBA NI PASUA KICHWA