YANGA 2-0 ASAS DJIBOUT

MCHEZO wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Azam Complex ubao unasoma Yanga 2-0 ASAS Djibout.

Ni dakika 45 za burudani kwa Wananchi ambapo wameshuhidia bao la kwanza likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 7 akiwa ndani ya 18.

Kazi ya pili inayowapeleka Yanga mapumziko wakiwa mbele ni mguu wa Konkoni dakika ya 44 akiwa ndani ya 18.

Yanga inahitaji kulinda ushindi ndani ya dakika 45 kusonga mbele katika hatua inayofuata Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuwa kwa sasa jumla ni mabao 4-0.