KASI YA LIGI ISIPOE, KAZI JUU YA KAZI

  LIGI Kuu Bara ambayo ilianza kwa kasi kutokana na maandalizi ambayo yalifanywa na timu zote. Ni burudani iliyokuwa imekosekana kwa muda na sasa ni msimu mpya.

  Ipo wazi kuwa kabla ya ligi kusimama mashabiki walipata ile ladha ya mpira waliyoikosa kwa muda. Hakika pongezi kwa wachezaji namna walivyoanza kwa kujituma kusaka ushindi.

  Muda uliopo kwa sasa ligi imesimama kutokana na timu za taifa kuwa na majukumu kwenye mechi za kuwania kufuzu AFCON hili ni jambo muhimu na kubwa kwetu pia.

  Haina maana mapumziko haya yawatoe kwenye ile kasi iliyoanza hakika haitapendeza bali ni muhimu kuendelea kufanya maandalizi ili kasi isizime ligi itakaporejea.

  Muda uliopo sio mrefu lazima itafika tarehe husika na ligi itaendelea hivyo jambo la msingi kwa kila timu kufanya maandalizi mazuri.

  Kila timu inahitaji matokeo mazuri kwenye mechi zake zote na haya ili yatokee ni muhimu kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati.

  Wapo wachezaji ambao wapo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata na wengine wapo kwenye majukumu ya timu ya taifa baada ya majina yao kutajwa.

  Wengine watakuwa katika masuala ya kifamilia kwa muda huu kutokana na ruhusa ambazo watakuwa walizipata katika timu zao yote yana umuhimu kufanyika kwa wakati.

  Ligi itakaporejea ile kasi iliyoanza kwenye mechi za mwanzo haitapaswa kuzimwa bali ule ushindani uzidi kuongezeka. Ili kuwa na mwendelezo mzuri ni muhimu kufanya maandalizi kwenye kila idara.

  Benchi la ufundi kwa mechi hizi za mwanzo kuna mapungufu ambayo yameonekana hapo ni muhimu kufanyia kazi ili ligi itakapoanza kuwe na mabadiliko kwenye maeneo ambayo hayakuwa sawa.

  Ikiwa kila mmoja atatimiza majukumu yake kwa wakati likizo hii itakuwa na manufaa makubwa kwa kila mmoja ambaye atatimiza kile kinachostahili.

  Wale ambao watapuuzia ukweli utakuwa wazi kwani mpira haufichiki ni mchezo wa wazi kila kitu kitaonekana ndani ya dakika 90 za ushindani kwenye kutafuta matokeo.

  Kikubwa ni kila mmoja kufanya kazi kwa juhudi kwa kuwa muda hausubiri na ligi msimu huu ushindani wake ni mkubwa.

  Kwa wachezaji ni muhimu kuwa tayari wakati wote. Kwenye mechi za kitaifa na kimataifa kila mashindano ambayo wanashiriki wanajukumu la kujituma kutiafuta ushindi.

  Wanapaswa watambue kwamba kuna nguvu kubwa kwenye kujituma na kufanya kazi kwa juhudi isiyo ya kawaida.

  Mashabiki furaha yao ni kuona wachezaji wanacheza kwa umakini na kupata matokeo chanya ambayo yanaleta furaha kwa kila mmoja.

  Kuanzia benchi la ufundi, mashabiki, viongozi na hata wachezaji wenyewe wanapenda kuona kila wanachokifanya kinakwenda vizuri na kwa wakati.

  Ikawe hivyo kwa muda uliopo hasa wale ambao hawajaitwa kwenye timu ya taifa wana muda wa kuendelea kujifunza kuwa bora zaidi.

  Kwa waliopo kwenye majukumu ya taifa nao wanapaswa kufanya kweli kupambania nembo ya timu ya taifa ili kupata matokeo mazuri.

  Kila kitu kinawezekana ikiwa kutakuwa na nia ya dhati kwenye kulitimiza jambo husika kwa wachezaji pamoja na viongozi bila kuwasahau mashabiki.

  Previous articleSTARS KAZINI LEO, SARE TU AFCON HII HAPA
  Next articleHISTORIA IMEANDIKWA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUFUZU AFCON