Home Sports HISTORIA IMEANDIKWA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUFUZU AFCON

HISTORIA IMEANDIKWA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS KUFUZU AFCON

HISTORIA nyingine imeandikwa baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kufuzu mashindano ya Afrika kwa timu za Taifa, (Afcon) yatakayofanyika Ivory Coast, Januari 2024.

Baada ya ubao kusoma Algeria 0-0 Tanzania ni pointi 8 wanafikia Tanzania wakiwa nafasi ya pili na Algeria nafasi ya Kwanza pointi 16 zote zimefuzu Afcon.

Kama wangepoteza mchezo huo kete huenda ingekuwa Kwa Uganda walishinda mabao 2-0 Niger.

Hongera kwa wachezaji zimetolewa na watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu ambaye amesema..”Mmeandika historia kwani hii ni mara yetu ya 3 kufuzu tangu kuanzishwa Kwa mashindano haya. Nawatakia kila la Kheri,”.

Previous articleKASI YA LIGI ISIPOE, KAZI JUU YA KAZI
Next articleMAXI, PACOME WAITEKA RWANDA,ROERTINHO ASHUSHA NONDO NZITO KWA LUIS