Home Sports STARS KAZINI LEO, SARE TU AFCON HII HAPA

STARS KAZINI LEO, SARE TU AFCON HII HAPA

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Algeria.

Katika mchezo huu wa leo kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrka, (AFCON 2023).

Stars inahitaji sare ikiwa kundi G inashika nafasi ya pili baada ya kucheza mechi tano na kukusanya pointi saba na Algeria ni vinara wana pointi 15.

Uganda ni nafasi ya tatu pointi zao kibindoni ni nne na mchezo huo unatarajiwa kuchezwa usiku saa nne Uwanja wa Mei 1956 uliopo Annaba, Algeria.

Wachezaji wamebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mshambuliaji John Bocco amesema kuwa watajituma kutafuta ushindi kwenye mchezo wa leo.

“Maandalizi ambayo tumefanya ni mazuri na wachezaji tupo tayari kwa ajili ya kuona timu inapata ushindi hivyo mashabiki wazidi kutuombea dua,”.

Previous articleNBC YAZINDUA NEMBO MPYA YA CHAMPIONSHIP
Next articleKASI YA LIGI ISIPOE, KAZI JUU YA KAZI