Home Sports WABABE KAZINI NA REKODI ZAO MATATA HIZI HAPA

WABABE KAZINI NA REKODI ZAO MATATA HIZI HAPA

MSAKO wa pointi tatu kwenye Ligi Kuu Bara unazidi kupamba moto huku kila timu zikionyesha uimara wake katika kutumia makosa ya wapinzani.

Septemba 21 itabaki kwenye rekodi kwa wababe wanne kuwa kazi kusaka ushindi na mwisho wawili wakawapoteza wapinzani wao.

Hapa tunakuletea namka kazi ilivyokuwa namna hii:-

Mabao ya mapema

Mashabiki wa Simba walishuhudia bao la mapema lililofungwa na Jean Baleke dakika ya 6 dhidi ya Coastal Union. Bao hilo lilikuwa ni la tatu kwa Baleke kufunga akitumia pasi ya Clatous Chama.

Kwa mashabiki waliokuwa Uwanja wa Azam Complex walishuhudia bao la Cheikh Sidibe dakika ya 10 kwa pigo huru akiwa nje ya 18 ambalo lilimshinda mlinda mlango Beno Kakolanya wa Singida Fountain Gate.

Bao la usiku

Ni Iddy Suleiman, (Nado) alipachika bao la usiku kwenye mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate ilikuwa dakika ya 90 akiwa ndani ya 18 baada ya mabeki wa timu pinzani kujichanganya kwenye kuokoa hatari.

Hat trick

Hat trick ya pili ilipatikana ndani ya ligi Uwanja wa Uhuru kupitia kwa Baleke ambaye alitupia mabao matatu kimiani.

Hat trick ya kwanza ilipatikana Uwanja wa Azam Complex na mtupiaji alikuwa ni Feisal Salum wa Azam FC alipowatungua Tabora United.

Pointi tatu

Timu mbili zilikomba pointi tatu mazima, ilikuwa ni Simba 3-0 Coastal Union na Azam FC 2-1 Singida Fountain Gate Uwanja wa Azam Complex. Wababe wote walioshinda walikuwa nyumbani.

Kadi nyekundu

Ni Uwanja wa Uhuru ulishuhudia mwamuzi wa kati Ahmed Arajiga dakika ya 19 alimuonyesha kadi ya moja kwa moja nyota wa Coastal Union Haji Uganda baada ya kuonekana akimchezea faulo Henock Inonga.

Inonga hakufanikisha mpango kazi wa kukomba dakika 90 alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Temeke kupatiwa matibabu zaidi ya mguu wa kulia ambao ulipata maumivu.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Simba, Abbas Ally alisema kuwa nyota huyo anapatiwa matibabu ili kurejea kwenye ubora.

“Jeraha ambalo alipata ni kubwa hivyo baada ya vipimo vikubwa zaidi itajulikana kuhusu aina ya matibabu ambayo atapata lakini baada ya kuumia alipata matibabu na anaendelea vizuri,”.

Walikutana na njano

Jina la kocha wa Azam FC, Yusuph Dabo linaingia kwenye orodha ya waliooyeshwa kadi za njano huku kwa wachezaji baadhi ni Greyson Gwalala wa Coastal Union ilikuwa dakika ya 13, Che Malone wa Simba dakika ya 45.

Uhuru na Azam Complex

Kwenye mechi mbili za wababe hawa waliokuwa kwenye msako wa pointi tatu, mabao sita yalikusanywa.Uwanja wa Uhuru ulikusanya mabao matatu na Uwanja wa Azam Complex ulikusanya mabao matatu.

Singinda Fountain Gate wakiwa ugenini waliambulia bao moja huku wakishuhudia wakifungwa mabao mawili baada ya dakika 90.

Mapigo huru

Mabao mawili ni mapigo huru ambapo ni Simba walianza dakika ya 40 kupitia kwa Baleke aliyepiga penalti iliyosababishwa na Luis Miquissone kuchezewa faulo ndani ya 18.

Chidibe alifuata ndani ya Azam Complex alipopiga pigo huru akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto na kumpoteza Kakolanya.

Bao la maajabu

Nyota wa Singida Fountain Gate, Marouf Tchakei kwa mguu wake wa kulia alipachika bao la maajabu ambalo Idrisu Abdulai hakutarajia kama angelijaza mazima ndani ya nyavu kutokana na eneo ambalo alikuwa nje ya 18.

Previous articleBOSI SIMBA AMPA TUZO JEAN BALEKE
Next articleKIMATAIFA KAZI BADO KUBWA IPO MBELE YA WAWAKILISHI