Home Uncategorized BOSI SIMBA AMPA TUZO JEAN BALEKE

BOSI SIMBA AMPA TUZO JEAN BALEKE

AKIWA na mabao matano kibindoni mshambuliaji wa Simba Jean Baleke amepewa kiatu cha ufungaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24.

Ni Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa kwa namna mshambuliaji huyo alivyo na kasi ya kufunga kuna nafasi kubwa kwa nyota huyo kuwa mfungaji bora.

Baleke timu ya kwanza kuifunga ilikuwa ni Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu, timu ya pili ilikuwa Dodoma Jiji ambapo aliwafunga bao mojamoja na Coastal Union ni timu ya tatu aliitungua mabao matatu.

Ally amesema: “Ni wazi kuwa kwa kasi ambayo ameanza nayo Baleke ana nafasi kubwa ya kutwaa kiatu cha dhahabu hilo analiweza na tunaamini itakuwa hivyo.

“Kwenye mechi ambazo tunacheza nafasi zinatengenezwa na wachezaji wanapambana kutimiza majukumu yao hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa kuna mechi zinakuja mipango yetu ni kupata matokeo mazuri,”.

Simba imekusanya pointi tisa kwenye ligi baada ya kucheza mechi tatu, safu ya ushambuliaji imetupia mabao tisa ile ya ulinzi imetunguliwa mabao mawili.

Previous articleGAMONDI AJA NA MPANGO KAZI WA KUVURUGAVURUGA
Next articleWABABE KAZINI NA REKODI ZAO MATATA HIZI HAPA