SUALA LA MIKATABA LINAHITAJI UMAKINI

  WACHEZAJI wengi kwenye timu mbalimbali Bongo wamekutana na Thank You kutokana na kile ambacho viongozi wameaona ilipaswa kufanyika hivyo.

  Sio Simba, Yanga, Azam FC, Singida Fountain Gate mpaka Geita Gold kuna wachezaji ambao walikutana na mkono wa asante.

  Pia kuna timu ambazo zilikutana na adhabu kutokana na kushindwa kuwalipa wachezaji ama makocha baada ya kuachana nao hili linahitaji umakini kwenye kuvunja mikataba.

  Wapo wale ambao wameachwa kutokana na kanadarasi kugota mwisho licha ya kuwa na uwezo mkubwa bado waliondoka katika timu husika.

  Kwa namna moja ama nyingine mchezaji kuondoka bure kwenye timu aliyodumu kwa muda akiwa na ubora wake uleule hii ni hasara kwa kuwa hakuna kitakachorejea kwa timu zaidi ya kuwa faida kwa mchezaji mwenyewe.

  Hiana maana kwamba ni lazima wachezaji wote wapewe mikataba ndipo wauzwe hapana, muhimu timu kuangalia ubora wa wachezaji wao pamoja na maboresho ya mikataba ili hata kama anaondoka fungu lingine libaki kwao.

  Ipo wazi kuwa uendeshaji wa timu ni gharama kubwa na kuwaacha wachezaji kuondoka bure ni mwendelezo wa kuongeza gharama husika.

  Ukiweka kando wale ambao mikataa yao inagota mwisho wapo wale ambao mikataba yao inasitishwa kwa makubaliano ya pande mbili

  Hili nalo linahitaji umakini mkubwa kulingana na gharama ambayo inakwenda kutokea. Kikubwa ni mpango mkakati mzuri kwenye hili unahitajika.

  Katika mikataba ya wachezaji suala la kuvunja mkataba nalo linapaswa liwepo kulingana na sababu ambazo timu itakuwa na faida nazo pamoja na mchezaji.

  Ikitokea mchezaji anaamua kuvunja mkataba ama timu inahitaji kuvunja mkataba basi iwe ni kwa mujibu wa vipengele vlivyopo na sio maamuzi ya mtu Fulani ama kiongozi.

  Hili litaepusha gharama zisizo za lazima pamoja na migogoro inayowaondoa wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwenye kupambania kombe.

   

  Previous articleINGIZO JIPYA SIMBA LAANZA MATIZI
  Next articleMASHINDANO YA AFL KUFANYIKA OKTOBA, UZINDUZI WA KIHISTORIA