Home Uncategorized MASHINDANO YA AFL KUFANYIKA OKTOBA, UZINDUZI WA KIHISTORIA

MASHINDANO YA AFL KUFANYIKA OKTOBA, UZINDUZI WA KIHISTORIA

MASHINDANO ya klabu bora barani Afrika, African Footal League , (AFL) yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 2023, uzinduzi wake wake unatarajiwa kufanyika Dar, Tanzania.

Ni mechi ya kwanza inatarajiwa kuchezwa Dar Oktoba 20,2023 ikiwa ni fursa kwa wachezaji bora Afrika kuonyesha uwezo wao kwenye ulimwengu wa michezo duniani.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanzia katika hatia ya robo fainali kisha hatua ya nusu fainali itafuata kati ya Oktoba 29 2023 au Novemba Mosi.

AFL ni ushirikiano wa kati ya CAF na FIFA imeundwa kwa misingi ya mechi za nyumbani na ugenini yatahusisha timu 8 bora barani Afrika kutoka kanda tatu za Kaskazini, Afrika ya Kati na Magharibi na Ukanda wa Kusini Mashariki.

Ni Al Ahly SC, Tunisia’s Esperance, Wydad Casablanca kutoka Morocco, Enyimba ya Nigeria, TP Mazembe ya DR Congo ndio vilabu kutoka Ukanda wa Kati Magharibi.

Mamelod Sundowns, ya Afrika Kusini, Angola’s Petro Atletico do Luanda na Klabu ya Simba ya Tanzania ni vilabu kutoka ukanda wa Kusini Mashariki.

Droo ya uzinduzi inatarajiwa kufanyika Cairo, Misri Septemba 2 2023 na yatafanyika kwa muda wa wiki nne huku mechi ya fainali ikitarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 5-11 2023.

Previous articleSUALA LA MIKATABA LINAHITAJI UMAKINI
Next articleGAMONDI ASHUSHA NONDO 5 YANGA, ROBERTINHO ANGIA ANGA ZA GAMONDI