
MAYELE ATAJA IDADI YA MABAO ANAYOTAKA KUFUNGA
FISTON Mayele, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hesabu zake kubwa ni kuona kwamba anaweza kufunga mabao kuanzia 20 jambo ambalo litaipa timu hiyo mafanikio. Kwa sasa mshambuliaji huyo ametupia mabao mawili kwenye ligi aliwafunga KMC na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mayele amesema kuwa anafurahi kufunga na anatarajia kufunga mabao mengi zaidi…