>

NYOTA HAWA WA SIMBA KUIKOSA NAMUNGO KESHO

MAMBO yanazidi kuwa magumu kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kutokana na kuanza kwa mwendo wa kusuasa msimu wa 2021/22 jambo ambalo linapoteza tabasamu kwa mashabiki wa timu hiyo.

Ikiwa ipo kwenye maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo, kesho Novemba 4, Uwanja wa Mkapa kuna orodha ya mastaa ambao wataukosa mchezo huo.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amewataja Pape Sakho, Mzamiru Yassin, Chris Mugalu na Taddeo Lwanga kwamba wataukosa mchezo huo.

Sababu ya nyota hao kuukosa mchezo huo ni kutokuwa fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo waliyapata kwenye mechi walizokuwa wakicheza.

Aidha beki wa kupanda na kushuka katika kikosi hocho Henock Inonga naye ataukosa mchezo huo kwa kuwa ana adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.