Home International CONTE ATAMBULISHWA NDANI YA TOTTENHAM

CONTE ATAMBULISHWA NDANI YA TOTTENHAM

BREAKING:Antonio Conte amerejea ndani ya Ligi Kuu England na atakuwa ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Hotspur inayoshiriki ligi hiyo pendwa duniani.

 

Conte anachukua mikoba ya Nuno Espirito ambaye alichimbishwa katika kikosi hicho jana Novemba kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo kwa kile kilichoelezwa kuwa ameshindwa kufikia malengo ya timu hiyo.

Mazungumzo na kocha huyo yalianza kufanyika jana ambapo alikwenda London kuweza kumalizana na mabosi hao na leo Jumanne, Novemba 2 amepewa dili la kuinoa timu hiyo.

Ni kandarasi ya miezi 18 ambayo amesaini na kuna kipengele cha kuweza kumuongezea mkataba mwingine kwa mara nyingine tena ikiwa atafanya vizuri kocha huyo mwenye miaka 52 na aliwahi kuifundisha Chelsea mwaka 2016-17 na alitwaa taji la Ligi Kuu England, FA  mara ya mwisho alikuwa ndani ya Inter Milan ambapo alitwaa taji la Serie A.

Previous articleNYOTA HAWA WA SIMBA KUIKOSA NAMUNGO KESHO
Next articleJESHI LA YANGA LEO DHIDI YA RUVU SHOOTING