MBAPPE ANACHEKA NDOTO YAKE KUTIMIA

INGIZO jipya ndani ya Real Madrid, Kylian Mbappe ambaye ameletwa duniani Desemba 20 1998 amebainisha kuwa ndoto yake imetimia.

Kwa muda mrefu tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa mwamba huyo ambaye ana rekodi ya kufunga hat trick katika fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina alikuwa kwenye rada za Real Madrid.

Hatimaye dili limejibu kwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa ambaye alikuwa anakipiga PSG kwa sasa changamoto mpya ni ndani ya Real Madrid.

Ipo wazi kwamba Madrid ni mabingwa mara 15 wa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo anaungana nao kuendelea kutimiza majukumu yake.

Nyota huyo amesema: “Ndoto imekuwa kweli, nina furaha sana na kujivunia kujiunga na klabu ya ndoto yangu Real Madrid. Hakuna ambaye anaweza kuelewa furaha niliyonayo kwa sasa “