Home International CHELSEA WAMEKIWASHA HUKO

CHELSEA WAMEKIWASHA HUKO

CHELSEA ni kicheko mwanzo mwisho baada ya kushuhudia ubao ukisoma Chelsea 6-0 Everton kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Mabao ya Cole Palmer aliyekuwa katika ubora wake na alitupia mabao manne ilikuwa dakika ya 13, 18, 29, 64 kwa mkwaju wa penalti.

Nicolas Jackson alitupia bao moja dakika ya 44 sawa na Alfie Gilchrist dakika ya 90 katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Stamford Bridge.

Sasa Chelsea inafikisha pointi 47 ikiwa nafasi ya 9 huku Everton ikiwa nafasi ya 16 na pointi zake 27.

Vinara ni Manchester City wanapointi 73 kibindoni huku Arsenal ikiwa nafasi ya pili pointi 71 sawa na Liverpool iliyo nafasi ya 3 zote zimecheza mechi 32 ndani ya tatu bora.

Previous articleAZAM FC SIO KINYONGE UJUE
Next articleNani ni Nani Leo Usiku wa Ulaya?