Home Sports AZAM FC SIO KINYONGE UJUE

AZAM FC SIO KINYONGE UJUE

MATAJIRI wa Dar Azam FC sio kinyonge ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na kasi wanayokwenda nayo kwenye mechi za ushindani msimu wa 2023/24.

Timu hiyo imekuwa kwenye ubora ndani ya uwanja kutokana na rekodi bora inazopata na mchezo wake uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukisoma Namungo 0-2 Azam FC mabao yote yakifungwa na Kipre Junior.

Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani uliopo nao wapo tayari kuwa kwenye mwendelezo mzuri wa kutafuta matokeo.

“Ligi ni ngumu ipo wazi kwa kuwa kila timu inapambana kupata matokeo mazuri nasi tunafanya hivyo kikubwa kila mchezo kwetu ni kuhakikisha kwamba tunapata matokeo mazuri.

“Wachezaji wanajituma na benchi la ufundi linafanya kazi yake kwa ukamilifu, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mechi zetu zote,”.

Azam FC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 50 baada ya kucheza mechi 22.

Previous articleHAWA WAKALI KWENYE KUFUNGA NA KUTOA PASI, MSHAMBULIAJI MMOJA
Next articleCHELSEA WAMEKIWASHA HUKO