Home Sports YANGA:HATUPOI, MWENDO ULEULE

YANGA:HATUPOI, MWENDO ULEULE

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi raia wa Tunissia amesema kuwa wanahitaji pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa leo Novemba 3, Uwanja wa Mkapa.

 

Manara amebainisha kwamba kikubwa ambacho wanahitaji ni kuendelea na kasi yao ileile ya kucheza na kushinda mechi za ligi kwa kuwa nia ipo na uwezo pia upo kutokana na wachezaji kupewa mafunzo makini.

Ameongeza kwa kusema kwamba mashabiki wamekuwa wakiwapa nguvu kubwa wachezaji hivyo waendelee kufanya hivyo na inawezekana kuona wakiendelea pale ambapo wameshia.

“Kwa namna ambavyo mashabiki wamekuwa wapo bega kwa bega na timu hapo kuna kitu ambacho wamekiongeza kwa mashabiki na kila mmoja anapenda hali hiyo hivyo mashabiki wasichoke waendelee kushangilia.

“Palepale ambapo tumeishia yaani kasiyetu haitapoa wale ambao wanafikiri kwamba timu itakata upepo basi hadithi hiyo wasahau huu ni wakati mwingine na mwaka mwingine kabisa.

“Kikubwa ni kuwa na utulivu na kuona mpira wa pasi nyingi ukipigwa kila mchezaji anajua hilo kocha wetu ni mzuri sana anawajua wachezaji wake na namna ya kuwatumia tunahitaji kukusanya pointi kwenye kila mchezo,” amesema.

Yanga imeshinda mechi zake nne mfululizo kwa msimu wa 2021/22 ikiwa ni mwendo mzuri kwa timu hiyo inayopigia hesabu taji la Ligi Kuu Bara.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi nne imekusanya pointi 12 na imetupia mabao 6.

Previous articleRUVU YAPANIA KUTIBUA REKODI YA YANGA KWA MKAPA
Next articleNYOTA HAWA WA SIMBA KUIKOSA NAMUNGO KESHO