ISHU YA MAKAMBO KUSUGUA BENCHI YAMEIBUKA HAYA
BAADA ya Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo kushindwa kuanza katika mchezo hata mmoja kikosini hapo msimu huu, kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ameweka wazi sababu za nyota huyo kushindwa kupenya kikosi cha kwanza. Makambo tangu atue Yanga msimu huu, ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza katika michezo mitano ya ligi kuu, huku akimuacha Fiston Mayele akitamba. Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema sababu kubwa ya Makambo kushindwa kucheza ni kutokana…