Home Sports KUMBE TATIZO LA AZAM FC LIPO HAPA

KUMBE TATIZO LA AZAM FC LIPO HAPA

VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa tatizo kubwa ambalo linaitesa timu hiyo kwenye mechi zake za ligi ni kukosa umakini kwenye mechi ambazo wamecheza.

Azam FC ilinyooshwa mabao 2-0 dhidi ya Yanga pia ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mechi za awali kabisa msimu wa 2021/22.

Ilishinda bao 1-0 mbele ya Geita Gold, Uwanja wa Azam Complex na ilikosa pia penalti kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa huku soka la kubutuabutua likitawala.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bahati amesema kuwa tatizo ambalo wameligundua kwenye mechi walizocheza ni kukosa umakini kwa wachezaji wao kwenye kutumia nafasi jambo ambalo wanalifanyia kazi.

“Ujue ligi ya msimu huu ni ngumu na kila timu inaingia uwanjani ikiwa inahitaji kushinda, kwa namna yoyote ile tatizo kubwa ambalo linatusumbua ni umakini kwenye safu ya ushambuliaji pamoja na ulinzi kuweza kuruhusu mabao.

“Kwa namna yoyote ile kwa kuwa tunahitaji kufanya vizuri tumefanyia kazi makosa hayo ili kupata matokeo kwenye mechi zijazo inawezekana mashabiki wasikate tamaa kila kitu kitakuwa sawa,” amesema Bahati.

Kwenye msimamo Azam FC ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi saba baada ya kucheza jumla ya mechi tano huku safu ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao manne na imefungwa mabao matano.

Previous articleSIMBA:MAGUMU TUNAYOPITIA YATAKWISHA
Next articleEXCLUSIVE:VIGOGO SIMBA WAVAMIA NYUMBANI KWA KIBWANA,NDANI YA CHAMPIONI IJUMAA