KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu,Steve Barker kimewasili Zanzibar leo Aprili 22, 2026 kwa maandalizi ya mwisho mchezo wa robo fainali Muungano Cup.
Timu hiyo inatarajiwa kutupa kete yake ya kwanza Aprili 23, 2026 itakuwa dhidi ya Mafunzo SC, saa 2:15 usiku.
Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga SC ambao wamefungua ukurasa kwa kupata ushindi wa magoli 4-0 Muembe Makuti robo fainali iliyochezwa Aprili 21, 2026.
Katika msafara wa Simba SC wapo wachezaji wote muhimu akiwemo Clatous Chama, Ellie Mpanzu, Duchu, Rushine, Seleman Mwalimu, Hussen Abel, Kibabage, Morice Abraham.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.