Home Sports NAMUNGO YATAJA KILICHOWAPONZA MBELE YA SIMBA KWA MKAPA

NAMUNGO YATAJA KILICHOWAPONZA MBELE YA SIMBA KWA MKAPA

HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kilichowaponza kupoteza pointi tatu mbele ya Simba ni umakini mdogo kwa wachezaji wake mwisho baada ya kuamini kwamba kazi imeisha.

Katika mchezo wa tano wa timu hizo mbili, ulipigwa mpira mkubwa Uwanja wa Mkapa na mpaka dakika ya 90 ngoma ilikuwa ni nzito kwa timu zote mbili hivyo iliwalazimu Simba kupata bao la ushindi katika dakika zile za nyongeza.

Morocco amesema:-“Lack of concentration is among of causes of Namungo to be beaten by Simba,(kupoteza umakini kwa wachezaji wangu kumefanya tukapoteza mbele ya Simba).

“Tulianza kwa kasi kipindi cha kwanza na tukakubaliana kwamba inabidi tuzuie kwa kuwa Simba ilikuwa na hasira hasa baada ya kushindwa kupata matokeo kwenye mechi yao iliyopita.

“Mpango kazi ulikubali kipindi cha kwanza tukarudi tena kipindi cha pili. Lakini sasa nguvu ilipungua baada ya mchezaji wetu mmoja kuonyeshwa kadi nyekundu.

“Yote kwa yote naweza kusema kwamba nawapongeza Simba kwa kuwa wameshinda nasi tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo kwani ligi bado haijaisha na tupo kwenye mpango wa kuendelea kupata ushindi,”.

Novemba 3, ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ulisoma Simba 1-0 Namungo na bao la Simba lilifungwa na Meddie Kagere ambaye alitoka benchi na kuchukua nafasi ya nahodha John Bocco.

Previous articleMSIMAMO WA LIGI KUU BARA BONGO
Next articleUNAI ATAJWA NEWCASTLE UNITED