UNAI Emery, Kocha Mkuu wa Villarreal amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba Klabu ya Newcastle United inaonekana kumuhitaji licha ya kwamba hawajapeleka ofa kwa wakati huu.
Kocha huyo inaelezwa kuwa atachukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa Newcastle United, Steve Bruce ambaye alifungashiwa virago kwenye timu hiyo baada ya timu hiyo kupata wawekezaji wapya mwezi uliomeguka.
Kwa sasa bado ana mkataba na Villarreal ambao utamfanya adumu hapo mpaka mwaka 2023 hivyo mabosi wa timu hiyo wanapaswa wajipange kuvunja mkataba wake ikiwa kweli wanahitaji saini yake.
Unai mwenyewe amesema kuwa Newcastle wamekuwa na nia naye hizo taarifa zipo lakini hakuna ofa ambayo ameipokea mpaka sasa yeye binafsi ama klabu yake hivyo hana la kusema ndiyo ama hapana katika hilo.
“Newcatle wamekuwa na nia na mimi, hizo taarifa zipo. Lakini hakuna ofa ambayo imekuja kwangu au kwa klabu yangu hivyo hakuna chochote cha kusema ndiyo au hapana,”.