Home Sports AZAM FC YAZITAKA POINTI TATU ZA GEITA GOLD

AZAM FC YAZITAKA POINTI TATU ZA GEITA GOLD

VIVIER Bahati,  Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Yanga matokeo wamesahahu hivyo hesabu zao ni kupata ushindi mbele ya Geita Gold ambao nao wamebainisha kuwa wanahitaji ushindi.
Azam FC imetoka kuambulia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Yanga, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa inatarajiwa kucheza na Geita Gold, leo Novemba 2,  Uwanja wa Azam Complex.
Akiizungumza na Saleh Jembe, Bahati amesema kuwa wanatambua wapinzani wao wapo imara na wana uwezo mkubwa uwanjani lakini hilo haliwapi tabu kwa sababu wanahitaji kupata matokeo.
“Tumesahau kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga akili zetu ni kuelekea mchezo dhidi ya Geita Gold na tunajua kwamba utakuwa mgumu ila tunachohitaji ni pointi tatu na ligi ni ngumu hilo tunajua,”
Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara Azam FC ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi nne huku Geita Gold ikiwa nafasi ya 13 na pointi 2 zote zimecheza mechi 4.
Kinara wa ligi ni Yanga ambaye kibindoni ana pointi 12 ikiwa imefunga mabao sita na safu ya ulinzi haijaruhusu bao mpaka sasa.
Previous articleMRITHI WA MIKOBA YA GOMES SIMBA HUYU HAPA
Next articleGEITA GOLD WATUMA UJUMBE HUU AZAM FC