>

GEITA GOLD WATUMA UJUMBE HUU AZAM FC

KUELEKEA kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya Geita Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex uongozi wa Geita Gold umeweka wazi kuwa unahitaji pointi tatu kwenye mchezo huo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Felix Minziro,  Kaimu Kocha Mkuu wa Geita Gold amesema kuwa waliwatazama Azam FC katika mechi zilizopita hivyo wataingia kwa mbinu tofauti kuwakabili.
Minziro amesema:-“Azam FC ni timu imara na nzuri kwa kuwa tuliiona katika mechi zilizopita kuelekea katika mchezo wetu tunawaheshimu ila tunahitaji pointi tatu muhimu.
“Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunaamini kwamba utakuwa ni mchezo mgumu lakini jambo ni moja tu ambalo tunahitaji pointi tatu.
“Matokeo mazuri ni kitu pekee ambacho wanakihitaji kuona kwamba tunashinda, tunajua kwamba Azam FC ni timu bora na nzuri hilo lipo wazi.
“Mashabiki wa Geita Gold wajue kwamba kazi yetu ni kuwapa burudani na hatutawaangusha kwa kuwa hata wachezaji wanajua nasi pia tunajua kwamba tunahitaji ushindi, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwa nasi bega kwa bega,”.