MRITHI WA MIKOBA YA GOMES SIMBA HUYU HAPA

IMEELEZWA kuwa Rhulani Mokwena ni moja ya makocha ambao wanapewa chapuo la kuibuka ndani ya kikosi cha Simba.

 

Kocha huyo ambaye anaifundisha Mamelodi Sundowns anaweza kuja kuchukua mikoba ya Didier Gomes ambaye alibwaga manyanga.

Mbali na jina la Mokwena pia Mserbia Milovan Cirkovic na Zdravko Logarusic pamoja na Josef Zinnbauer kocha wa zamani wa Orlando Pirates naye anatajwa kuingia kwenye rada za Simba.

Kwa sasa kikosi cha Simba kipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Hitimana Thiery akiwa na msaidizi wake Seleman Matola.

Tayari wameweza kuongoza kwenye mechi mbili za ligi ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania ambapo Simba ilishinda bao 1-0 na mchezo wa pili ulikuwa mbele ya Coastal Union kwenye sare ya bila kufungana.

Kesho Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Namungo FC kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.