CONTE KUSAINI DILI JIPYA LEO TOTTENHAM

ANTONIO Conte anatarajiwa kusaini dili jipya leo Jumanne ili kuweza kuwa Kocha Mkuu wa Tottenham.

Conte anakwenda kuchukua mikoba ya Nuno Espirito ambaye alichimbishwa mazima jana Novemba Mosi.

Espirito alifungashiwa virago kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo ambapo kwenye mechi zake sita za Ligi Kuu England alipoteza mechi nne.

Kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Manchester United akiwa nyumbani kiliwafanya mabosi wa timu hiyo kushindwa kuvumilia na kufanya iwe ni rekodi ya kumtimua kocha wa nne ndani ya miaka mitatu.