LWANDAMINA BADO YUPOYUPO SANA AZAM

LICHA ya kuwa na matokeo mabaya msimu huu Kocha Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja wa kuzidi kukinoa kikosi hicho. Lwandamina alijiunga na Azam msimu uliopita baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha mkuu Mromania, Aristica Cioaba.

 

Mpaka sasa Azam imecheza mechi nne za ligi huku akishinda moja dhidi ya Namungo kwa bao 1-0, wakatoka sare na Coastal Union ya 1-1, wakafugwa mabao 2-1 na Polisi Tanzania na walipokutana na  Yanga  wakakubali ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Yanga 2-0 Azam FC.

 

Azam pia imetolewa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufugwa bao 1-0 na Pyramid kwenye mchezo wa marudiano baada ya suluhu Uwanja wa Chamazi.

 

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:-“Kiukweli sina taarifa kama kocha anataka kufukuzwa ndiyo maana hizo ni tetesi ila hakuna hata mpango wakuondolewa.

“Mkataba wake umeisha na atasaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia Azam,” alisema ofisa habari huyo.