ARGUERO ASHAURIWA KUKAA NJE MIEZI MITATU

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Barcelona, Sergio Arguero  atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu ikiaminika kuwa ni kutokana na kusumbuliwa na tatizo la moyo.

 

Nyota huyo ambaye ameibuka ndani ya kikosi hicho kinachoshoshiriki La Liga akitokea Klabu ya Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu England alipata tatizo hilo Oktoba 30 wakati timu hiyo ilipokuwa ikivaana na Alaves kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania.

Katika mchezo huo nyota huyo alilalala chini na kushika kifua huku akieleza kuwa alikuwa anashindwa kupumua lakini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na madaktari wamemtaka mchezaji huyo kupumzika kwa muda wa miezi mitatu bila kugusa mpira.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Camp Nou ubao ulisoma Barcelona 1-1 Alaves na watupiaji kwa Barcelona alikuwa ni Memphis Depay dakika ya 49 na Luis Rioja kwa Alaves ilikuwa dakika ya 52 na kuwafanya wagawane pointi mojamoja.