RED ARROWS WAPINZANI WA SIMBA WANA MCHECHETO
WAPINZANI wa Simba katika Kombe la Shirikisho barani Afrika, Klabu ya Red Arrows imeweka wazi kuwa nia yao ya kusonga mbele katika michuano hiyo huku wakitamba kufanya vizuri wakiwa ugenini. Red Arrows kutoka Zambia Jumapili Novemba 28 watacheza mchezo wao wa kwanza wa mtoano wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika Desemba Mosi nchini Zambia ambapo Simba watakuwa ugenini…