Home Sports DODOMA JIJI KAZINI LEO KUWAKABILI VINARA WA LIGI

DODOMA JIJI KAZINI LEO KUWAKABILI VINARA WA LIGI

LIGI Kuu Tanzania Bara leo Mei 15,2022 inaendelea ambapo vinara Yanga wanatarajiwa kumenyana na Dodoma Jiji.

Wakiwa na pointi 57, Yanga watamenyana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 8 na pointi 28.

Timu zote zimecheza mechi 23 hivyo utakuwa ni mchezo wao wa 24 ndani ya msimu wa 2021/22.

Kocha Mkuu wa Yanga,Nasreddine Nabi amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wanahitaji matokeo.

“Tumeshindwa kupata matokeo kwenye mechi zetu za hivi karibuni hilo linatosha hivyo mbele ya Dodoma Jiji tupo tayari kwa ajili ya kupata ushindi na tutapambana kuona hilo linatokea,”.

Masoud Djuma, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema wanawaheshimu wapinzani wao Yanga ila wataingia kwa tahadhari ili kupata ushindi.

Previous articleCHEKI NYOTA WALIOKOSA PENALTI BONGO
Next articleHII HAPA RATIBA YA LIGI KUU BARA