Home Sports CHEKI NYOTA WALIOKOSA PENALTI BONGO

CHEKI NYOTA WALIOKOSA PENALTI BONGO

LIKIWEKWA tuta,asilimia 98 wengi wanahesabu ngoma lazima ijae wavuni lakini kuna mastaa wengi ambao wamekwama kufanya hivyo kwenye uwanja.

Kitete cha kutetema hakikuwa kwa Fiston Mayele tu msimu huu hata Meddie Kagere wa Simba alipata kitete cha kufunga.

Rekodi zinaonyesha kwamba kitete cha penalti kipo kwa mastaa wa Simba ambao wamekosa penalti nyingi,hapa tunakuletea baadhi ya mastaa ambao walikosa kwenye ligi namna hii:-

Mastaa watano kutoka Simba

Mastaa watano ndani ya kikosi cha Simba walikwama kufunga penalti ikiwa ni pamoja na Rally Bwalya mbele ya Azam FC, John Bocco mbele ya Biashara United, Erasto Nyoni mbele ya Ruvu Shooting, Chris Mugalu alikosa mbele ya Mbeya City na Meddie Kagere alikosa mbele ya Biashara United.

Lakini ikumbukwe kwamba Kagere ndani ya dakika 90 aliwahi kufunga kwa mkwaju wa penalti mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na Bwalya aliwahi kufunga mbele ya Polisi Tanzania.

Hivyo kwa msimu huu wa 2021/22 mastaa wa Simba wamekuwa kwenye kigugumizi katika kujaza kimiani penalti ambazo wanazipata ndani ya uwanja.

Pablo Franco,Kocha Mkuu wa Simba aliliambia Championi Jumamosi kuwa huwa inatokea wachezaji kushindwa kutumia mipira ya mapigo huru jambo ambalo linafanyiwa kazi.

Mayele

Mei 9,2022 wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 0-0 Prisons itakuwa kwenye kichwa cha Fiston Mayele pamoja na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wanaamini kwamba atafikisha bao la 13 ila alikwama kumtungua Hussein Abel.

Penalti iliyosababishwa na Feisal Salum baada ya kuchezewa faulo ndani ya 18 dk ya 37 na jukumu la penalti likawa miguuni mwa Mayele yeye alikosa.

Inakuwa ni penalti ya kwanza kwake msimu huu kwenye ligi kukosa kwa kuwa katika mabao yake 12 aliyonayo hajafunga kwa penalti.

Nasreddine Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga alisema kuwa Mayele hakupanga kukosa penalti hiyo ila ilitokea kama ambavyo huwa inatokea kwa wachezaji wengine.

Boban na Masota

Oktoba 16,2021 ilikuwa ni siku ya makipa kuonyesha uwezo wao wa kuokoa penalti,ambapo Uwanja wa Nyankumbu ulisoma Geita Gold 1-1 Mtibwa Sugar.

Kila timu ilipata nafasi ya penalti ni Mtibwa Sugar walianza kupata dk ya 29 ikakoswa na Boban Zirintusa baada ya kipa Benedickt Tinocco kuweza kuokoa.

Pia Geita Gold nao walipata penalti na mpigaji alikuwa ni Raymond Masota mikono ya Aboutwalib Mshery ambaye kwa sasa yupo Yanga aliweza kuipangua penalti hiyo.

Mwaikenda

Lusajo Mwaikenda wa Azam FC hakuwa na bahati ya kufunga ilikuwa mbele ya Geita Gold na msababishaji wa penalti hiyo alikuwa ni kiungo mshambuliaji Idd Seleman,’Nado’.

Ilikuwa ni Novemba 2,2021 Uwanja wa Azam Complex penalti hiyo iliokolewa na mikono ya Khomeny Aboubakar ila Azam FC ilishinda bao 1-0.

Ambokile

Staa wa Mbeya City,Eliud Ambokile hakuwa na bahati ya kufunga penalti ilikuwa mbele ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

Ubao uliweza kusoma Mbeya City2-2 Mbeya Kwanza na kipa wa Mbeya Kwanza aliyeweza kupangua penalti hiyo anaitwa Hamad Juma.

Previous articleTEN HAG ATUMIWA UJUMBE NA RONALDO
Next articleDODOMA JIJI KAZINI LEO KUWAKABILI VINARA WA LIGI