JOHN BOCCO KWENYE KIBARUA KIGUMU SIMBA

     MSIMU wa 2021/22, nahodha wa Simba John Bocco ametupia mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara ambayo imekuwa na ushindani mkubwa.

    Bao lake la kwanza alifunga mbele ya Ruvu Shooting kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni baada ya kupitia msoto wa muda mrefu bila kufunga.

    Bao lake la pili alifunga mbele ya Kagera Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

    Mabao yake yote mawili katupia Uwanja wa Mkapa na Simba iliweza kukusanya pointi sita katika msako wa pointi sita uwanjani.

    Ikumbukwe kwamba ni staa wa kwanza ndani ya Simba kukosa penalti ilikuwa ni mbele ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara na timu zote ziligawana pointi mojamoja.

    Ana kazi nzito kuweza kufikia idadi ya mabao 16 aliyofunga msimu uliopita akiwa na deni la mabao 14 kuweza kufunga kwa sasa na ligi ikiwa inakaribia kufika ukingon.

    Ana kazi ya kutetea kiatu cha ufungaji bora kwa kuwa msimu wa 2020/21 ambapo alitupia mabao 16 na pasi mbili.

    Bao la 16 alifunga mbele ya Namungo, Uwanja wa Mkapa ilikuwa kwa mkwaju wa penalti ambao aliusababisha yeye mwenyewe alipotokea benchi.

    Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa moja ya washambuliaji wazuri na wenye uwezo ni pamoja na nahodha huyo mzawa.

    Previous articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
    Next articleLIGI KUU BARA RATIBA