Home Uncategorized MASTAA YANGA WAFUNGUKIA KUTOPENDA SARE

MASTAA YANGA WAFUNGUKIA KUTOPENDA SARE

BAADA ya msoto wa kuambulia sare kwenye mechi tatu mfululizo,wachezaji wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi wameweka wazi kwamba hawajapenda kupata sare.

Yanga ilianza kuambulia sare mbele ya Simba ilikuwa Aprili 30 kisha ngoma ikawa Ruvu Shooting 0-0 Yanga na kigogo cha tatu ilikuwa ni Yanga 0-0 Tanzania Prisons.

Aboutwalib Mshery,kipa namba mbili wa Yanga alisema kuwa matokeo ambayo wameyapata kwenye mechi zilizopita hawajapenda hivyo watapambana kushinda mechi zijazo.

“Kupata sare sisi hatujapenda lakini kwa kuwa ni matokeo basi tutazidi kupambana kwa mechi zijazo ili kuweza kushindwa kwani mechi bado zipo na tunaamini kwamba tutashinda,”.

Mkongwe Deus Kaseke alisema:”Tumepata sare mechi zilizopita hilo lishapita sasa tunaangalia mbele kwa ajili ya kupata pointi tatu kazi bado haijaisha na tutazidi kupambana,”.

Dickson Ambundo winga wa Yanga alisema;”Akili zetu ni kwa mechi zetu zijazo, sare zimeupa somo kuweza kufanya vizuri kwa mechi zijazo lakini hayakuwa malengo yetu,” alisema.

Leo,Yanga inatarajiwa kumenyana na Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.

Previous articleSAUTI:MAYELE ATANGAZA HALI NYINGINE,APANIA KUFUNGA
Next articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA DODOMA JIJI HIKI HAPA