Hapa ndipo kambi ya Yanga SC itakapokuwa

MABINGWA watetezi wa NBC Premier League kwa msimu mpya wa 2026/27 wamebainisha watakapoweka kambi kwa maandalizi ya msimu ujao.

Ikumbukwe kwamba Yanga SC wametwaa ubingwa wakiwapoteza kwa pointi 2 wapinzani wao wa karibu Simba SC, ni pointi 75 walikusanya baada ya mechi 30 huku Simba SC wakiwa na pointi 73.

Kuelekea kwenye maandalizi ya msimu ujao, timu hiyo itaweka kambi Avic Town Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ali Kamwe, amesema kocha mpya amehitaji wachezaji wote kuripoti kambini Julai 20 mwaka huu.

Hii ni kawaida kwa timu hiyo, kuweka kambi yao Avic Town badala ya kwenda nje ya nchi kama zinavyopenda kufanya timu nyingine.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.