
SIMBA YAFANYA KIKAO NA KOCHA MPYA SAA 72
NDANI ya Championi Jumatano habari kubwa inaeleza kuwa wakati Pablo akitimuliwa, Simba SC yafanya kikao na kocha mpya kwa saa 72
NDANI ya Championi Jumatano habari kubwa inaeleza kuwa wakati Pablo akitimuliwa, Simba SC yafanya kikao na kocha mpya kwa saa 72
LEO Mei 31 Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Pablo Franco Martin raia wa Hispania. Katika taarifa iliyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, imeeleza kuwa katika kipindi chote cha kumalizia msimu, timu itakuwa chini ya kocha msaidizi, Seleman Matola. Taarifa hiyo imeongeza kuwa pia…
MABINGWA wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni Wydad baada ya kushinda mabao 2-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mohamed V. Linakuwa ni taji la tatu kwa timu hiyo ya Morroco kuweza kutwaa baada ya kuanza kufanya hivyo 1992 na 2017. Zouhair El Moutaraji aliweza kuwa shujaa kwenye mchezo wa fainali ya…
MWENDO ambao unaendelea kwa sasa kwenye ligi ni lazima kila mmoja aweze kupambania kile ambacho anakitaka kwa kuwa hakuna timu inayokubali kufungwa. Kila mechi inayochezwa imekuwa na ushindani mkubwa na hili ni jambo la muhimu kwa kila mmoja kukubali kile ambacho kinatokea. Ikitokea timu ikafungwa kwa makosa yao basi inapaswa kukubali hali halisi kwamba imepoteza…
UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba umeondoa matumaini yote ambayo walikuwa nayo watani wao wa jadi Simba kutwaa mataji msimu huu. Simba ilikuwa inatetea taji la Kombe la Shirikisho na kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga. Kwenye upande wa Ligi Kuu…
PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba anatarajiwa kukutana leo na uongozi wa Simba ili kuweza kuzungumza kuhusu mwendo wake ndani ya kikosi hicho. Kocha huyo baada ya kurithi mikoba ya Didier Gomes malengo yote ambayo alikabidhiwa na timu yameyeyuka jumlajumla jambo linalofanya nafasi yake kuwa kwenye wakati mgumu. Moja ya malengo ilikuwa ni kutetea mataji yaliyokuwa…
POLISI Tanzania wamendeleza kasi ya msako wa pointi tatu baada ya kushinda kwa mabao 2-0 Biashara United. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Ushirika Moshi,Mei 30 uliwafanya mastaa wa Polisi Tanzania kuwa na furaha baada ya ushindi huo. Ni ushindi wa pili mfululizo Polisi Tanzania inashinda baada ya kushinda mbele mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar….
STAA wa Liverpool, Sadio Mane ametangaza kuondoka ndani ya kikosi hicho msimu ujao wa 2023/24 hivyo hatakuwa miongoni mwa wale ambao watashiriki Ligi Kuu England akiwa na timu hiyo. Nyota huyo ambaye ni kiungo raia wa Senegal anatajwa kutua ndani ya kikosi cha Bayern Munich. Nyota huyo alitoa maamuzi yake ya kuondoka ndani ya Liverpool…
IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ipo kwenye hesabu za kuwania saini ya Mustafa Kiza. Nyota huyu ni beki raia wa Ugada hivyo anakuja kuongeza nguvu kwenye upande wa ulinzi ndani ya kikosi hicho. Yanga imekuwa imara kwenye upande wa mabeki msimu huu ikiwa ni timu namba moja iliyofungwa mabao…
BEKI wa Simba, Shomari Kapombe ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa kucheza na Niger na nafasi yake imechukuliwa na Lusajo Mwaikenda wa Azam FC. Kapombe ameondolewa kwenye kikosi cha Stars kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyopata wakati akiwa ndani ya kikosi cha Simba. Nyota huyo aliumia kwenye mchezo wa…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumanne
LEO Mei 30,2022 Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na mchezaji wake Saido Ntibazonkiza baada ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miwili. Katika taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga,imeeleza kuwa Ntibazonkiza amemaliza utumishi wake ndani ya klabu hiyo. Taarifa hiyo imeeleza namna hii:”Uongozi wa Klabu ya Yanga unapenda kutoa shukrani za…
WACHEZAJI watatu wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco wanawania tuzo ya mchezaji bora. Tuzo hiyo ni maalumu kwa ajili ya mashabiki ambao wamekuwa wakichagua mchezaji kupitia njia ya mtandao kwa kumpigia kura mchezaji wanayempenda ili aweze kusepa na tuzo hiyo. Ni kiungo mzawa Mzamiru Yassin kiungo wa kazi, Rally Bwalya pia…
PONGEZI kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17, Serengeti Girls kwa kuweza kutanguliza mguu mmoja hatua ya kufuzu Kombe la Dunia. Ushindi walioupata nchini Cameroon una maana kubwa hivyo ni zamu yao kuweza kuendeleza ule mwendo ambao wameanza nao bila kuchoka. Tuna amini kwamba mchezo wa marudio utatoa picha…
RASMI Klabu ya DTB itatumia jina la Singida Big Star baada ya kulitangaza leo Mei 30,2022 na itahamisha makazi kutoka Dar mpaka Singida. Mtendaji Mkuu wa Singida Big Star, Muhibu Kanu amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wameamua kubadili jina kutokana na suala la biashara pamoja na uwekezaji. “Tumeamua kubadili jina kutoka DTB na…
RAIS wa Heshima ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, Mo ametoa kauli nyingine ya matumaini akiweka wazi kwamba lazima wafanyie kazi maboresho ya maeneo ambayo yanamadhaifu. Simba imepoteza malengo ya kutwaa ubingwa baada ya kuzidiwa pointi 13 na watani zao wa jadi Yanga huku ikiwa imetoka kupoteza taji la Kombe la Shirikisho baada ya…
PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba anatajwa kuwa kwenye hesabu za kufutwa kazi kutokana na mwendo wa kusuasua wa timu hiyo. Habari zinaeleza kuwa kauli ya Rais wa Heshima wa Simba, Mohamed Dewji kwamba Simba wanapaswa kuchukua maamuzi magumu ni pamoja na kusafisha benchi la ufundi. Ikumbukwe kwamba baada ya Simba kufungwa bao 1-0 dhidi…