Home Sports MO ATOA KAULI NYINGINE SIMBA YA MAAMUZI

MO ATOA KAULI NYINGINE SIMBA YA MAAMUZI

RAIS wa Heshima ndani ya Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, Mo ametoa kauli nyingine ya matumaini akiweka wazi kwamba lazima wafanyie kazi maboresho ya maeneo ambayo yanamadhaifu.

Simba imepoteza malengo ya kutwaa ubingwa baada ya kuzidiwa pointi 13 na watani zao wa jadi Yanga huku ikiwa imetoka kupoteza taji la Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali na Yanga.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Simba ilifungwa bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Feisal Salum.

 Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mo ameandika ujumbe huu:”Kwa ujumla miaka 5 iliyopita imekuwa ya mafanikio kwa Simba. Bajeti iliongezeka mara 5, tulishinda makombe mengi ya ndani na tuliweka alama kimataifa kwa kufika robo fainali tatu za michuano ya Afrika.

” Najivunia kuweza kusema tupo katika orodha ya vilabu bora 12 Afrika. Hii imekuwa mara ya kwanza Simba kuwa na mwendelezo mzuri katika miaka 86 ya historia yetu. Hakuna kurudi nyuma, tunatakiwa kufanya mabadiliko katika maeneo ambayo tuna madhaifu na kwenda mbele. Mapambano yanaendelea,”.

Previous articleYANGA YAMPONZA PABLO SIMBA
Next articleDTB SASA NI SINGIDA BIG STARS,WATAMBULISHA KIONGOZI MPYA