Home Sports DTB SASA NI SINGIDA BIG STARS,WATAMBULISHA KIONGOZI MPYA

DTB SASA NI SINGIDA BIG STARS,WATAMBULISHA KIONGOZI MPYA

RASMI Klabu ya DTB itatumia jina la Singida Big Star baada ya kulitangaza leo Mei 30,2022 na itahamisha makazi kutoka Dar mpaka Singida.

Mtendaji Mkuu wa Singida Big Star, Muhibu Kanu amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wameamua kubadili jina kutokana na suala la biashara pamoja na uwekezaji.

“Tumeamua kubadili jina kutoka DTB na sasa itakuwa inaitwa Singida Big Star hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kwa kuwa mipango yote imefuata utaratibu na hakuna ambacho kitaharibika.

“Kuhusu makazi tutakuwa Singida tunaipelekea timu hiyo huko kwa kuwa hakukuwa na timu ambayo inashiriki ligi na tunawapelekea burudani wakazi wa Singida.

“Uwanja wa Liti utakuwa kwa ajili ya mechi ambazo tutakuwa nyumbani hivyo tumejipanga kufanya vizuri tunawashukuru wale ambao wamekuwa pamoja nasi kila wakati tangu Championship na sasa ndani ya ligi tutafanya vizuri.

“Pia tutakuwa na Ofisa Habari ambaye tutafanya naye kazi anaitwa Hussein Massanza huyu anatambulishwa leo na atakuwa pamoja kwenye kazi yetu na timu,”

Previous articleMO ATOA KAULI NYINGINE SIMBA YA MAAMUZI
Next articleTUWEKEZE NGUVU KUBWA SOKA LA WANAWAKE