Home Sports TUWEKEZE NGUVU KUBWA SOKA LA WANAWAKE

TUWEKEZE NGUVU KUBWA SOKA LA WANAWAKE

PONGEZI kubwa kwa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17, Serengeti Girls kwa kuweza kutanguliza mguu mmoja hatua ya kufuzu Kombe la Dunia.

Ushindi walioupata nchini Cameroon una maana kubwa hivyo ni zamu yao kuweza kuendeleza ule mwendo ambao wameanza nao bila kuchoka.

Tuna amini kwamba mchezo wa marudio utatoa picha ya wapi ambapo tutakuwa lakini Imani yetu ni kuona kwamba timu inasonga mbele zaidi.

Kwa namna ambavyo maandalizi yameanza kwa mara nyingine tena tunaona kwamba kwa mechi zijazo kila kitu kitakuwa sawa na bendera itawakilishwa bila makosa.

Katika ulimwengu wa soka la Wanawake Tanzania tunaona  wamekuwa wakifanya vizuri na hii ina maana uwekezaji ukiongezwa hapa kila kitu kitakwenda kuwa na matokeo mazuri kwenye mashindano yote ambayo watakuwa wanashiriki.

Kwa namna ambavyo watakuwa wanafanya vizuri kwenye mechi ambazo wanacheza wanafungua milango ya kufanya vizuri kimataifa.

Hilo litwafanya waweze kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania na hapo unakuwa ni mwendelezo wa kuwafanya wazidi kuwa imara wakati wote.

Ipo wazi kwamba miongoni mwa timu ambazo zimeleta mataji mengi na muhimu kila pale ambapo walikuwa wakienda kushiriki huwezi kuiweka kando timu ya Taifa ya Wanawake.

Yote haya yanawezekana kutokana na uwekezaji ambao umekuwa ukifanyika hasa kwenye soka la Wanawake ambalo kwa Tanzania linazidi kukua kwa kasi.

Yapo mengi ambayo yanapaswa kuboreshwa ili kuweza kupiga hatua kubwa zaidi ya hapa na kinachohitajika ni kuweza kuongeza nguvu na kuzifanya hizi timu kuweza kuwa na uimara katika uchumi.

Pia wakati huu Twiga Stars nao wapo kwenye maandalizi kwa ajili ya kushiriki CECAFA hawa nao wapewe ushirikiano mkubwa na maandalizi yao yawe imara zaidi.

Kwa namna ambavyo wameanza maandalizi kwa sasa mpaka itakapofika Juni muda wa mashindano yanayotarajiwa kufanyika nchii Uganda tuna amini kutakuwa na kitu kizuri kimepatikana.

Kwa wale ambao wanaendelea kuwekeza huku ni jambo jema na muhimu kwao kuweza kuendelea kuwa bega kwa bega na timu hizi.

Jambo la msingi kwa wachezaji ni kuzingatia maelekezo ya benchi la ufundi na kufanya kile ambacho kitakuwa na faida kwa timu.

Watanzania tuzidi kushirikiana kwa ajili ya kuona timu hizi zinaweza kuwa mbali katika mafanikio hasa kwa kuzidi kuwa bega kwa bega hasa kwenye mechi za nyumbani na kuwaombea bila kuchoka.

Rai yangu kwa mashabiki kuweza kujitokeza kwa wingi pia hata pale Wanawake wanapokuwa wakicheza na hili litaongeza nguvu kwao kuweza kufanya vizuri zaidi na zaidi.

Kujitokeza kwa mashabiki kunaongeza nguvu kwa wachezaji kufurahia uwepo wa wale wanaojitokeza pamoja na kuzidi kujituma zaidi.

Tunajua kwamba Watanzania wanapenda mpira na wanapenda kuoa timu zikifanya vizuri hivyo ni muda wa kujitokeza sasa pale timu zetu zinapokuwa zinacheza.

Kila siku kwa wachezaji wanapokuwa uwanjani nao wanajukumu la kuwapa furaha mashabiki wale ambao watakuwa wamejitokeza uwanjani.

Jambo lao ni moja kucheza kwa kushirikiana na kuipa timu matokeo hilo ni muhimu kwa kila mchezaji kujua.

Ambacho kitawafanya mashabiki kujitokeza uwanjani ni matokeo mazuri na juhudi za kila mmoja kufanya vizuri kwenye mchezo husika.

Previous articleDTB SASA NI SINGIDA BIG STARS,WATAMBULISHA KIONGOZI MPYA
Next articleMASTAA WATATU SIMBA WAWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA