Home Sports YANGA YAMPONZA PABLO SIMBA

YANGA YAMPONZA PABLO SIMBA

 PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba anatajwa kuwa kwenye hesabu za kufutwa kazi kutokana na mwendo wa kusuasua wa timu hiyo.

Habari zinaeleza kuwa kauli ya Rais wa Heshima wa Simba, Mohamed Dewji kwamba Simba wanapaswa kuchukua maamuzi magumu ni pamoja na kusafisha benchi la ufundi.

Ikumbukwe kwamba baada ya Simba kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho wamepoteza malengo yote waliyokuwa nayo kwa msimu huu.

Ngao ya Jamii, Ligi ya Mabingwa wamekwama kutinga hatua ya robo fainali na kwenye Kombe la Shirikisho Afrika waligota hatua ya robo fainali na kwenye Kombe la Shirikisho walilokuwa wakitetea wameishia hatua ya nusu fainali.

Kauli ya Mo ilieleza kuwa wamekuwa kwenye msimu mbaya hivyo ni lazima wafanya maamuzi magumu kwa ajili ya msimu ujao.

Previous articleKLOPP ANAAMINI WATAREJEA WAKIWA BORA MSIMU UJAO
Next articleMO ATOA KAULI NYINGINE SIMBA YA MAAMUZI