Home Sports KLOPP ANAAMINI WATAREJEA WAKIWA BORA MSIMU UJAO

KLOPP ANAAMINI WATAREJEA WAKIWA BORA MSIMU UJAO

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa timu hiyo itarejea kwa kishindo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na kuweza kutwaa taji hilo.

Liverpool ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo ila ilipoteza kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Real Madrid kwa kufungwa bao 1-0 jijini Paris.

Licha ya kufungwa kwenye fainali hiyo juzi kipigo hicho kinaonekana kuwaumiza zaidi Liverpool kuliko kile walichopokea mwaka 2018 kwa kufungwa mabao 3-1 na Real Madrid.

Ikumbukwe kwamba 2019 walicheza kwa mara nyingine fainali na walishinda mabao 2-0 dhidi ya Tottenham sasa Klopp anataka historia ijirudie.

“Siyo vibaya kufika fainali tayari ni aina ya mafanikio ninaamini kwamba tutarejea tena hivyo ndivyo ilivyo kwa vijana wangu ni washindani wa kweli,” amesema.

Previous articleBAO LA FEI KWA SIMBA THAMANI YA BILIONI
Next articleYANGA YAMPONZA PABLO SIMBA