Home Sports WINGA MANE ATAJWA KUIBUKIA BAYERN MUNICH

WINGA MANE ATAJWA KUIBUKIA BAYERN MUNICH

STAA wa Liverpool, Sadio Mane ametangaza kuondoka ndani ya kikosi hicho msimu ujao wa 2023/24 hivyo hatakuwa miongoni mwa wale ambao watashiriki Ligi Kuu England akiwa na timu hiyo.

Nyota huyo ambaye ni kiungo raia wa Senegal anatajwa kutua ndani ya kikosi cha Bayern Munich.

Nyota huyo alitoa maamuzi yake ya kuondoka ndani ya Liverpool mara baada ya mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Kwenye mchezo huo Liverpool ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kushuhudia ubingwa ukienda Real Madrid.

Baada ya fainali hiyo ripoti zilieleza kuwa Mane yupo tayari kwa changamoto mpya na timu ambayo anatajwa kwenda ni Bayern Munich.

Previous articleBEKI HUYU AWEKWA RADA ZA YANGA
Next articlePOLISI TANZANIA YAIMALIZA BIASHARA UNITED