Home Sports POLISI TANZANIA YAIMALIZA BIASHARA UNITED

POLISI TANZANIA YAIMALIZA BIASHARA UNITED

POLISI Tanzania wamendeleza kasi ya msako wa pointi tatu baada ya kushinda kwa mabao 2-0 Biashara United.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Ushirika Moshi,Mei 30 uliwafanya mastaa wa Polisi Tanzania kuwa na furaha baada ya ushindi huo.

Ni ushindi wa pili mfululizo Polisi Tanzania inashinda baada ya kushinda mbele mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kwenye mchezo huo ni mabao ya Deusdedith Cosmas aliweza kufunga bao la utangulizi ilikuwa dk ya 31 na msumari wa mwisho ulipachikwa na nyota Tariq Seif dk ya 41 na kuimaliza biashara mapema ya msako wa pointi tatu.

Sasa Polisi Tanzania inafikisha pointi 33 ikiwa nafasi ya 7 huku Biashara United ikibakiwa na pointi zake 24 baada ya kucheza mechi 26.

Previous articleWINGA MANE ATAJWA KUIBUKIA BAYERN MUNICH
Next articlePABLO FRANCO KUKUTANA NA MABOSI SIMBA