Home Sports PABLO FRANCO KUKUTANA NA MABOSI SIMBA

PABLO FRANCO KUKUTANA NA MABOSI SIMBA

PABLO Franco,Kocha Mkuu wa Simba anatarajiwa kukutana leo na uongozi wa Simba ili kuweza kuzungumza kuhusu mwendo wake ndani ya kikosi hicho.

Kocha huyo baada ya kurithi mikoba ya Didier Gomes malengo yote ambayo alikabidhiwa na timu yameyeyuka jumlajumla jambo linalofanya nafasi yake kuwa kwenye wakati mgumu.

Moja ya malengo ilikuwa ni kutetea mataji yaliyokuwa mikononi mwa Simba lile la Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Tayari ameshavuliwa lile la Kombe la Shirikisho baada ya kuishia hatua ya nusu fainali na alifungwa mbele ya Yanga bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa Mei 28,2022 Uwanja wa CCM Kirumba.

Kwa upande wa taji la ligi ni ngumu kuweza kutwaa taji hilo kwa kuwa wameachwa kwa jumla ya pointi 13 na wapinzani wao Yanga walio nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 64.

Habari zimeeleza kuwa mabosi wa Simba baada ya kurejea kutoka Mwanza wameomba kukutana na Pablo ili waweze kuzungumza kuhusu mwendo wa timu hiyo na malengo kwa mechi zijazo.

Rais wa Heshima ndani ya Simba, Mohamed Dewji, ‘Mo’ baada ya timu hiyo kuondolewa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga alisema kuwa lazima wafanye maamuzi magumu

Previous articlePOLISI TANZANIA YAIMALIZA BIASHARA UNITED
Next articleYANGA:TUMEONDOA MATUMAINI YOTE YA SIMBA