Home Sports YANGA:TUMEONDOA MATUMAINI YOTE YA SIMBA

YANGA:TUMEONDOA MATUMAINI YOTE YA SIMBA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba umeondoa matumaini yote ambayo walikuwa nayo watani wao wa jadi Simba kutwaa mataji msimu huu.

Simba ilikuwa inatetea taji la Kombe la Shirikisho na kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Yanga.

Kwenye upande wa Ligi Kuu Bara Simba imeachwa kwa jumla ya pointi 13 na Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 64 kibindoni.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua kwamba matumaini ya Simba ilikuwa ni kutwaa Kombe la Shirikisho lakini hawana ujanja huo.

“Imekuwa ni ngumu kwao kuweza kufanya vizuri kwetu na matumaini yao ya kutwaa Kombe la Shirikisho yamekwenda hivyo wanakazi kubwa msimu huu.

“Tuliweka wazi kwamba mpango mkubwa ulikuwa ni kushinda na kuweza kutinga hatua ya fainali jambo la kwanza limetimia hivyo mpango ujao ni kufanya vizuri kwenye mechi zetu za ligi na mchezo wa fainali,”.

Yanga itacheza na Coastal Union kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuchezwa Julai 2,2022.

Previous articlePABLO FRANCO KUKUTANA NA MABOSI SIMBA
Next articleUKIFUNGWA LAZIMA UKUBALI MAISHA YAENDELEE