Home Uncategorized UKIFUNGWA LAZIMA UKUBALI MAISHA YAENDELEE

UKIFUNGWA LAZIMA UKUBALI MAISHA YAENDELEE

MWENDO ambao unaendelea kwa sasa kwenye ligi ni lazima kila mmoja aweze kupambania kile ambacho anakitaka kwa kuwa hakuna timu inayokubali kufungwa.

Kila mechi inayochezwa imekuwa na ushindani mkubwa na hili ni jambo la muhimu kwa kila mmoja kukubali kile ambacho kinatokea.

Ikitokea timu ikafungwa kwa makosa yao basi inapaswa kukubali hali halisi kwamba imepoteza mchezo na haina maana kwamba kwa mechi zijazo itapoteza.

Kila timu inahesabu za kushinda kwenye mechi zake hivyo jambo la msingi ni kuona kila mmoja anapata kile anachostahili.

Ukifungwa kubali na uweze kujipanga kwa ajili ya mechi zijazo na ajabu na kweli ni kwamba zipo timu ambazo wengi walikuwa hawatarajii zitashinda lakini zilishinda.

Kikubwa kwenye mchezo wa mpira kasumba ya kubeba matokeo mfukoni hiyo haitakiwi kwa kuwa kila mechi ni mpya kwa wachezaji wote pamoja na timu husika.

Mbinu za benchi la ufundi zitumike kwa ajili ya kusaka ushindi kwenye mechi hizi za lala salama kwenye ligi.

Waaamuzi umakini unahitajika kuendelea ili kuweza kupunguza makosa ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na imani yetu ni kuona kwa wakati huu wa lala salama matokeo yatapatikana kwa uhalali.

Kila la kheri wachezaji kwenye majukumu ya wakati huu ambapo kinachotakiwa ni mchezo wa kiungwana na kucheza kwa umakini mkubwa kwa kuwa wachezaji wanahitaji usalama.

Previous articleYANGA:TUMEONDOA MATUMAINI YOTE YA SIMBA
Next articleWAYDAD WATWAA TAJI LA TATU LIGI YA MABINGWA AFRIKA