Home Sports KAPOMBE AWEKWA KANDO TIMU YA TAIFA YA TANZANIA

KAPOMBE AWEKWA KANDO TIMU YA TAIFA YA TANZANIA

 BEKI wa Simba, Shomari Kapombe ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa kucheza na Niger na nafasi yake imechukuliwa na Lusajo Mwaikenda wa Azam FC.

Kapombe ameondolewa kwenye kikosi cha Stars kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyopata wakati akiwa ndani ya kikosi cha Simba.

Nyota huyo aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold uliochezwa Mei 22, Uwanja wa CCM Kirumba na waliweza kugawana pointi mojamoja baada ya kufungana bao 1-1.

Kapombe alianza kwenye mchezo huo lakini alikwama kukamilisha dk 90 baada ya kuumia na nafasi yake ilichukuliwa na Jimmsony Mwanuke.

Stars inatarajia kucheza Uwanja wa Stade de I’Amitie, Juni 4 mwaka huu dhidi ya Niger ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023.

Hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichopoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa nusu fainali, Kombe la Shirikisho.

Previous articleMRITHI WA PABLO ATUA DAR,NDANI YA SPOTI XTRA JUMANNE
Next articleBEKI HUYU AWEKWA RADA ZA YANGA